Kuali mbiu ya Open access week 2023: Kuipa Jamii kipaumbele dhidi ya Biashara

“Kuipa Jamii kipaumbele dhidi ya Biashara” ndio kauli mbiu ya mwaka huu katika International Open access week, (Oktoba 2023). Kauli mbiu hii inahimiza mazungumzo ya wazi kuhusu mbinu gani ambazo zinaweza kuendeleza na kupa kipaumbele uwazi katika usomi na kwa maslahi ya raia na kwa jamii ya kiusomi-na zile ambazo haziwezi kutumika.

Ikiwa imeidhinishwa na mataifa 193 wanachama, pendekezo la UNESCO kuhusu uwazi katika sayansi linasisitiza umuhimu wa kuipa jamii kipaumbele dhidi ya biashara katika wito wake wa kuzuia “kutokuwepo kwa usawa katika kupata faida kutoka kwa shughuli za kisayansi zinazofadhiliwa na umma”. Na kuunga mkono “modeli za uchapishaji zisizo za  kibiashara na za  uchapishaji shirikishi zisizotoza ada za utayarishaji wa makala. Kwa kuzingatia maeneo haya, tunaweza kufikia maono ya awali yaliyoainishwa wakati ambapo uwazi wa kujadili masuala ya utafiti yalipofafanuliwa. “mbinu za zamani na teknolojia mpya zimekutanishwa kwa ajili ya  manufaa ya umma ambayo hayajawai kushuhudiwa.

Maslahi ya kibiashara yanapopewa kipaumbele dhidi ya jamii ambayo utafiti unalenga kuhudumia, masuala mengi huibuka. Open access week hutuoa fursa kwa watu binafsi kujadili masuala muhimu katika muktadha wao. Haya ni pamoja na: Ni nini ambacho hupotea wakati ambao idadi inaendelea kudidimia ya mashirika yanayosimamia usambazaji wa maarifa kuliko watafiti wenyewe? Je, modeli ya kibiashara inayoimarisha viwango vya juu vya faida ina gharama zipi? Ni wakati upi ambapo ukusanyaji na matumizi ya data ya kibinafsi unaweza kudidimiza uhuru wa kitaaluma? Je, biashara katika taaluma inaweza kunufaisha umma? Je kuna mbinu mbadala zinazotumia miundombinu inayodhibitiwa na jamii ambayo tayari ipo na ambayo inaweza kunufaisha jamii ya watafiti na umma (kama vile nakala za awali, hifadhi ya data, na majukwaa huria ya uchapishaji)? Je, tunawezaje kubadilisha kutoka katika modeli ya awali ili kutumia modeli zinazolenga jamii.

Kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ilichaguliwa na kamati ya ushauri ya Open access week inatoa fursa ya kuungana pamoja, kuchukua hatua na kuhamasisha kuhusu umuhimu wa jamii kusimamia mifumo ya kusambaza maarifa. Hafla ya Open access week 2023, itafanyika kuanzia tarehe 23 hadi 29 Oktoba; Ingawa, yeyote anahimizwa kuandaa mijadala na kuchukua hatua inapohitajika mwaka huu na kutimiza kauli mbiu  na shughuli hii kulingana na muktadha wake.

Kwa habari zaidi kuhusu International Open access week, tafadhali rejelea tovuti ya openaccessweek.org.  Twiter hashtag rasmi #OAWeek

Previous
Previous

Română

Next
Next

Kishwahili (Tanzanian)