Kuali mbiu ya Open Access Week 2024 Inaendelea Wito wa “Jamii badala a Ubiasharishaji”

Mada ya International Open Access Week 2024 itaendelea na zingatio la mwaka uliyopita wa “Jamii badala a Ubiasharishaji.” Mada hii ilichangia katika utambulisho unaoendelea kuwa kuhusu hitaji la kuweka vipaumbele katika mbinu za kufungua elimu inayohudumia masilahi bora zaidi ya umma na jamii ya wataalam. Kuchukua hatua ambayo haikufanywa hapo awali ya kuendeleza mada hii katika mwaka wa pili inaangazia umuhimu wa mazungumzo haya na inatupatia fursa ya kubadilisha mazungumzo haya kuwa hatua ya pamoja.

Maswali mengi yaliyoibuliwa na mada hii mwaka uliyopita bado ni zenye umuhimu katika mwaka wa 2024 huku tukiangalia maendeleo ya mwisho zaidi, kama kasi ya kuongeza akili mnemba (artificial intelligence) katika mifumo ya kielimu bila ushauri wa jamii. Maswala yanayoendelea kuibuka ya kihakiki ni kama: Je athari ni zipi wakati idadi ndogo ya mashirika yanatawala uzalishaji wa elimu badala ya watafiti wenyewe? Je gharama fiche ni zipi za mifumo za kibiashara zinazotafuta mapato ya kupita kiasi huku zikipanua ukosefu wa usawa? Je ni lini ambapo ukusanyaji usiyo wazi na matumizi ya data ya kibinafsi na mashirika ya kibiashara utaanza kuharibu uhuru wa kielimu? Je ni lini na ni katika njia gani ambapo masilahi ya kibiashara inaweza kupatana na masilahi ya umma? Ni miundombinu zipi zinazotawaliwa na jamii zilizopo tayari zinazohudumia vizuri zaidi masilahi ya jamii ya watafiti na umma (kama seva za kupiga chapa mapema, hifadhi za utafiti, na jukwaa za kuchapisha za bure)? Je tunaweza kubadilisha fikra na kutumia zaidi chaguo hizi zinazoangazia jamii?

Majamii yanahimizwa kubadilisha mada ili ipatane zaidi kwa mazingira yao ya eneo na kuiongezea ili kuangazia mazungumzo maalum ambazo wangependelea kuzingatia. Mifano ya mazungumzo yanaweza kuwa “Jamii badala a Ubiasharishaji: Je Utawala wa Jamii ni nini & Mbona ni Muhimu,” “Jamii badala a Ubiasharishaji: Kuchukua Upya Uhuru wa Kielimu,” au “Jamii badala a Ubiasharishaji: Kuangazia Usawa katika Uzalishaji wa Elimu.” Violezo vya michoro vinavyoweza kubadilishwa yataweza kupatikana kwa jamii ili kuendeleza mada hizi zinazotumika kwa eneo.

Open Access Week 2024 itafanyika kutoka Oktoba tarehe 21 hadi 27; lakini mtu yeyote anahimizwa kuanzisha mazungumzo na kuchukua hatua wakati wowote unaofaa zaidi ndani ya mwaka. Ili kupata taarifa zaidi kuhusu Open Access Week, tafadhali tembelea openaccessweek.org. hashtag ya kirasmi ya wiki ni #OAWeek.

Tafsiri za tangazo hili katika lugha zingine zinaweza kupatikana katika openaccessweek.org. Michoro ya mada ya mwaka huu wa Open Access Week zinaweza kupatikana katika openaccessweek.org.

Kuhusu SPARC

SPARC ni shirika la utetezi haki isiyotafuta mapato inayotegemeza mifumo ya utafiti na elimu ambazo ziko wazi na zilizo na usawa katika mpango wao. Tunaamini kwamba kila mtu anapaswa kuwa na uwezo wa kupata na kuchangia katika elimu inayochagiza dunia yetu. International Open Access Week ilianzishwa na SPARC na washiriki wake katika jamii ya wanafunzi katika mwaka wa 2008. Jifunze zaidi katika sparcopen.org.

Kuhusu International Open Access Week

Open Access Week ni fursa yenye thamani kubwa zaidi ya kuunganishwa kwa harakati ya ulimwengu ya kuelekea kwa kugawana wazi wa elimu kwa kuendeleza mabadiliko katika sera na umuhimu wa maswala ya kijamii yanayowaathiri watu kote duniani. Tukio hili muhimu huadhimishwa na watu binafsi, taasisi, na mashirika kote duniani, na mpangilio wake huongozwa na kamati ya ushauri wa kimataifa, ambao huchagua mada ya kila mwaka each year’s theme. hashtag ya kirasmi ya Open Access Week ni #OAweek.

Previous
Previous

日本語

Next
Next

українська